WANAFUNZI WA TIA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PRETORIA

February 19, 2026

Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wamefanya ziara ya mafunzo na ubunifu katika Jiji la Pretoria, nchini Afrika Kusini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa taasisi wa kukuza ujasiriamali, ubunifu na ushindani wa kimataifa kwa wanafunzi wake.

Ziara hiyo iliwahusisha washindi wanane (8) kutoka kila kampasi waliopata ufadhili maalum baada ya kuibuka na mawazo bora ya biashara katika mashindano ya ubunifu yaliyoandaliwa na taasisi. Aidha, wanafunzi wengine walijigharamia kushiriki safari hiyo kwa lengo la kupata uzoefu wa kimataifa na kuongeza upeo wa maarifa katika kuendeleza mawazo yao ya kibiashara.

Katika ratiba ya ziara hiyo, wanafunzi walipata fursa ya kutembelea University of the Witwatersrand (Wits University), moja ya vyuo vikuu vinavyoongoza barani Afrika kwa tafiti na ubunifu. Wakiwa chuoni hapo, walijifunza kuhusu mifumo ya kuendeleza mawazo ya biashara kuanzia hatua ya ubunifu hadi utekelezaji wake, pamoja na namna taasisi za elimu zinavyoshirikiana na sekta binafsi kukuza teknolojia na ujasiriamali.

Aidha, wanafunzi walitembelea The Innovation Hub, kituo cha ubunifu na maendeleo ya teknolojia kilichopo Pretoria. Kupitia mawasilisho na majadiliano na wataalamu wa kituo hicho, walipata uelewa kuhusu programu za incubation na acceleration, upatikanaji wa mitaji kwa wabunifu, na umuhimu wa mitandao ya kimataifa katika kukuza biashara changa (startups).

Ziara hiyo pia ilihusisha kujifunza kuhusu mifumo ya kisasa ya digital library na digitalization, ambapo wanafunzi walishuhudia namna teknolojia inavyotumika kuboresha upatikanaji wa taarifa na kusaidia tafiti, ubunifu na maendeleo ya kielimu.

Kupitia ziara hii, wanafunzi wa TIA wameongeza uelewa, ari na maono mapana ya kibiashara, huku taasisi ikiendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuandaa wahitimu wenye maarifa, ubunifu na uwezo wa kushindana katika soko la ajira na biashara ndani na nje ya nchi. Ziara hii ni hatua muhimu katika safari ya kuimarisha ubunifu na kukuza uchumi kupitia mawazo ya vijana wabunifu.

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/