WATAALAMU WA WIZARA YA ELIMU WAKAGUA UJENZI WA JENGO LA TAALUMA TIA SINGIDA

April 2, 2025

Wataalamu wa Ujenzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wamefanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la taaluma katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida.

Katika ukaguzi huo, wataalamu hao wakiongozwa na Mhandisi Hanington Kagiraki, Msanifu Majengo Dickson Haule, na Mkadiriaji Majengo Geofrey Nyaluke walikagua hatua mbalimbali za ujenzi wa jengo hilo la kisasa ambalo linatarajiwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wa TIA.

Jengo hilo la ghorofa tatu linajumuisha madarasa ya kisasa, ofisi, na kumbi za mihadhara, likiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3,600 kwa wakati mmoja. Mradi huu unatekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya Mpango wa HEET kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 13.

Wakizungumza baada ya ukaguzi, wataalamu hao walieleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo huku wakisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kazi inakamilika kwa viwango vya juu na ndani ya muda uliopangwa.

Mradi huu unatarajiwa kuwa chachu ya kuboresha elimu ya uhasibu na biashara kwa kutoa mazingira bora ya kujifunzia, hivyo kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

 

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/