Waratibu wa masuala ya Jamii katika utekelezaji wa mradi wa HEET unaoendelea kwa Kampasi za Mwanza na Singida wametoa elimu ya mradi wa HEET katika kipindi chote cha utekelezaji huo.
Mratibu Sofia Venance amesema kipindi cha utekelezaji wa mradi ni muhimu wananchi kufahamu namna mradi utaavyotelezwa, jinsi malalamiko yatakavyoshughulikiwa na fursa zilizopo katika maeneo yanayozunguka miradi,
“Nawasihi tujiepushe na vishawishi vya wageni wa nje wanaokuja kufanya kazi na kuondoka kwa kutokuanzisha mauhusiano ambayo yanaweza pelekea ukapata mtoto na baadae ukatekelezwa ,”. Alisisitiza Mratibu Sofia
Naye, Mratibu Simon Wankogere amesema miradi hii inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita imelenga kutekelezwa bila kuathiri mazingira na endapo kutakuwa na changamoto yoyote ya kimazingira basi wananchi and wasisite kutoa taarifa katika ofisi ya malalamiko ili kupatiwa ufumbuzi.
“Ukiona mkarandasi hahafuata sheria za usalama mahala pa kazi, vibarua hawajalipwa, au changamoto yoyote ambayo inaweza kwamisha maendeleo ya utekelezaji wa mradi basi usisite kutoa taarifa,”. Alisisitiza Mratibu Simon