TIA YATOA MILIONI TATU KWA WAFANYAKAZI HODARI

May 2, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeungana na Wafanyakazi wengine nchini katika kuadhimisha  siku ya Wafanyakazi duniani kwa kuwazawadia wafanyakazi hodari kutoka kampasi zake zote jumla ya shilingi milioni tatu.
Waliopewa zawadi katika maadhimisho hayo ni John Sosthenes Mapuli,Mhadhiri Msaidizi Kampasi ya Dar es Salaam, Brown Masuba, Mkutubi Msaidizi Kampasi ya Mbeya, Prosper Tegamaisho, Mhadhiri Kampasi ya Singida, Siku Mbava, Msaidizi Mwendesha Ofisi Kampasi ya Mtwara, Vicent Msigala, Mhadhiri Msaidizi Kampasi ya Mwanza na  Kephas Paul Ugula, Mhadhiri Msaidizi Kampasi ya Kigoma.
Wafanyakazi hao wamepatiwa kiasi cha shilingi laki tano kila mmoja ikiwa ni wito kwa wafanyakazi wote kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni, huku wakizingatia weledi, ubunifu, uwajibikaji na ubora katika kutimiza majukumu yao.
Maadhimisho hayo ambayo kimkoa yamefanyika katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa Makao Makuu ya Taasisi, huku Kampasi za Mbeya, Mtwara, Singida, Mwanza na Kigoma zikiadhimisha katika Mikoa yao.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mishahara na Maslahi Bora kwa Wafanyakazi ndio Kilio chetu: Kazi Iendelee”
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/