TIA KIGOMA YAJIVUNIA UWEKEZAJI WA MIUNDOMBINU MPYA

December 6, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mhe. Rashid Chuachua, aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, amepongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza shilingi bilioni 11.08 katika ujenzi wa miundombinu ya kudumu ya Kampasi ya Kigoma. Ameeleza kuwa mradi huu, ambao umefikia asilimia 58 ya utekelezaji, utaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia huku ukipunguza gharama za upangaji wa majengo.

Mhe. Rashid Chuachua ameongeza kuwa Kampasi ya Kigoma sasa ina miundombinu ya kisasa ikiwemo madarasa ya kisasa, maktaba yenye teknolojia ya kisasa, maabara ya kompyuta, na ofisi za watumishi. Vyote hivi ni sehemu ya kuhakikisha wanachuo wanapata mazingira bora ya kujifunzia, jambo linaloonyesha dhamira ya Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri, Mjumbe wa Bodi, Profesa Mapesa, ameipongeza Serikali kwa juhudi hizi kubwa na kusisitiza umuhimu wa nidhamu, ubunifu, na ushirikiano kwa wahitimu. Amesema wahitimu wanapaswa kuwa mfano wa uongozi bora na kutumia elimu yao kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwa kutumia teknolojia na kuanzisha biashara zenye tija.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William Amos Pallangyo, amewahimiza wahitimu 794 wa mwaka huu kutumia elimu yao kwa maendeleo ya taifa. Amepongeza ongezeko kubwa la udahili wa wanachuo kwa asilimia 93.1 tangu kuanzishwa kwa kampasi hii mwaka 2014, akibainisha kuwa maendeleo haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali katika elimu.

Kampasi ya Kigoma imeendelea kutoa mchango mkubwa kwa jamii kupitia mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kwa kushirikiana na JA DEEP, ambapo wanachuo 450 walifaulu mitihani ya mtandaoni na kutunukiwa vyeti. Pia, imeendesha madarasa ya maandalizi ya mitihani ya CPA na CPSP pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam kwa wafanyabiashara wa Kigoma katika nyanja mbalimbali za biashara na uhasibu.

Mhuhitimu Elizabeth ndimchanga aliyepata GPA ya 5 wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi amesema kuwa amehitimu kwa furaha kubwa huku akiahidi kufanyia kazi wosia uliotolewa na viongozi. Aidha, amepongeza juhudi za ujenzi wa miundombinu mpya akiamini kuwa wahitimu wa baadae watafaidika zaidi kutokana na uboreshaji huu.

 

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/