Wanachuo na watumishi wa TIA  Kampasi ya Mwanza wamiminika  kuchangia damu leo, tarehe 13.04.2022 ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kampeni ya “kuchangia damu okoa Maisha leo” iliyoratibiwa na Meneja wa Kampasi hiyo Dkt. Honest Kimario akishirikiana na Afisa Rasilimali Watu wa Kampasi hiyo Ndugu Obeid Joseph.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali katika jamii ili kutatua changamoto zitakazojitokeza hususani hii ya upungufu wa damu