TIA Kampasi ya Mwanza imefanya wiki ya semina elekezi (Orientation) kwa Wanachuo wapya wa Cheti, Diploma na Shahada ya kwanza waliodahiliwa kwa mwaka wa Masomo 2022/2023 ambayo imeanza tarehe 31/10/2022 mpaka 4/11/2022.
Akiongea na wanachuo hao Dkt. Honest Kimario amewapongeza kwa kuchaguliwa kujiunga na TIA Kampasi ya Mwanza,
“Ukiulizia ni wapi naweza kupata elimu bora,
na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ni moja kati ya vyuo vitakavyotajwa katika kuhakikisha unapata elimu yenye ufanisi,”. Alisema Dkt. Kimario
Dkt.Kimario pia amesema lengo la semina hiyo ni kuwafahamisha wanachuo hao wapya taratibu, miongozo, sheria na kanuni mbalimbali zinazotumika katika utoaji wa elimu na ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zozote zitakazokuwa zinajitokeza.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imejikita kutoa elimu yenye ufanisi ambayo itamjenga Mwanachuo kujitegemea, kujiajiri na kuajiriwa.