Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kwa mamlaka aliyonayo
chini ya Kifungu cha 5(4) cha Sheria ya Wakala za Serikali, Sura 245, amefanya uteuzi
wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)
kama ifuatavyo: –
1. Amemteua Prof. Jehovaness Aikael kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Prof. Aikael ni Profesa Mshiriki, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam;