NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO BI.JENIFA OMOLO AFANYA ZIARA YA KIKAZI TIA 

September 5, 2022

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo leo amefanya ziara ya kikazi Katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ambapo ameipongeza taaisis hiyo kwa ujenzi wa Kampasi zake hasa Kampasi ya Mwanza na Mtwara ambazo zinatumia Majengo ya kukodi “hii itaiwezesha TIA kuepuka  kutumia kiasi kikubwa cha fedha za Serikali katika kukodi majengo hayo,”. Alisema Naibu Katibu Mkuu

Aidha, Bi. Jenifa Omolo amesema TIA iendelee kuboresha elimu ambayo inawajenga wanafunzi kujiajiri na si kutegemea ajira “Hongereni sana kwa kuongeza udahili hadi kufikia Wanachuo 25,388, ongezeko hili linaonesha kuwa Watanzania wanaimani na TIA, hivyo nataka niwasisitize ongezeko hili  liendane na ubora wa elimu  itakayomuwezesha mwanachuo kujiajiri,”. Alisisitiza Naibu Katibu Mkuu

 Afisa Mtendaji Mkuu Prof. William Pallangyo wakati akisoma taarifa yake amesema kuwa sasa TIA ina Kampasi 6 ambazo zimekaa kimkakati  Pwani (Dar es Salaam), Kanda ya Ziwa (Mwanza), Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kusini (Mtwara) Kanda ya Kati (Singida) na kwa sasa Taasisi imepata eneo Zanzibar Makunduchi ambapo itajenga Kampasi  ya Saba.

Prof. Pallangyo aliongeza kuwa Taasisi ipo mbioni kuanzisha tawi Dodoma ambapo ni makao makuu ya Nchi ili kuweza kuwafikia Wadau wake kwa urahisi, 

“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa Ufadhili  mkubwa  katika ujenzi  wa Miradi yetu ya Kimkakati inayoendelea katika kampasi zetu, ambapo kukamilika kwa miundombinu ya kusomea na kufundishia kutaiwezesha TIA kuongeza udahili,”. Alisema Prof. Pallangyo

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William A.Pallangyo alipowasili kwa ziara ya kikazi leo Septemba 05, 2022

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akisalimiana na Naibu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) anayeshughulikia  Mipango na Utawala Dkt. Isaya Hasanali (aliyevaa kaunda suti ya bluu) alipowasili kwa ziara ya kikazi leo Septemba 05, 2022.Wanaoshuhudia ni baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali za Menejiment ya TIA.

 

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akiweka sahihi kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mtendaji Mkuu wa TIA, alipofanya ziara ya kikazi leo Septemba 05, 2022. Aliye keti mbele yake ni Prof. William A.Palangyo, Afisa Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania.

Pichani ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William A.Pallangyo alipofanya ziara ya kikazi TIA, leo Septemba 05, 2022.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Prof. William A.Pallangyo akionesha mgawanyiko wa matawi ya TIA kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo kama ilivyobainishwa kwenye ramani ya Tanzania. Anayeshuhudia ni katibu wa Naibu katibu mkuu, bwana Amani Ngedu.

Eng.Masuhuko Nkuba, Estate Meneja wa TIA, akiwasilisha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TIA kwa ufadhili wa Serikali na Fedha za Taasisi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo alipotembelea TIA leo Septemba 05, 2022.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo (katikati) akifurahia jambo wakati wakati Meneja wa Miliki wa TIA, Eng. Masuhuko Nkuba akiwasilisha miradi inayotekelezwa na Taasisi, leo Septemba 05, 2022. Wa kwanza kulia ni Prof.William A.Pallangyo na wa kwanza kushoto ni bwana Amani Ngedu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William A. Pallangyo (aliye simama) akiwasilisha taarifa ya Taasisi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo alipotembelea TIA leo Septemba 05, 2022.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo (katikati) akisisitiza jambo wakati wakati alipokutana na Menejiment ya TIA, leo Septemba 05, 2022. Wa kwanza kulia ni Prof.William A.Pallangyo na wa kwanza kushoto ni bwana Amani Ngedu.

Dkt. Isaya Hasanali,(mwenye suti ya bluu) akitoa neno la shukrani kufuatia ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo – TIA, leo Septemba 05, 2022.

Menejiment ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ikiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo (wa pili kushoto waliokaa) alipotembelea TIA – TIA, leo Septemba 05, 2022.

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/