Afisa Mtendaji Mkuu Profesa William Pallangyo amewaasa wanachuo kuwa michezo ni furaha na Afya pia kwani kupitia michezo Afya ya akili uimarika sana hivyo kuwa chachu kubwa ya kufanya vizuri katika masomo yao,
“Pia wanamichezo muwe wabunifu kwa kutumia mbinu mbalimbali za michezo ili kupata ushindi katika timu unayoichezea,”. Amsema Profesa Pallangyo
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania William Palangyo alipokutana na wanachuo waliowasili Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano ya SHIMIVUTA.
Wanachuo wa TIA watashindania tuzo mbalimbali kupitia michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa wavu na riadha.
Naye Mlezi wa Wanachuo Lucina Comino amewasisitiza wanachuo hao kuepuka vitendo vyovyote ambavyo ni hatarishi katika kipindi chote watakachokuwa katika michezo hiyo,
“Tukiwa katika michezo yetu hii, nidhamu iwe ya hali ya juu na tutimize kile ambacho kimekusudiwa katika michezo na si tabia hatarishi ambazo zitaharibu sifa ya TIA,”. Alisema Madam Comino
Katika Michuoano inayoendelea Mechi za leo mpira wa miguu kati ya LGT na TIA huku TIA wakiibuka kidedea kwa goli 1, upande wa mpira wa kikapu TIA wameshinda kwa vikapu 53 dhidi ya Mw.nyerere vikapu 46.