Kikao hicho kilijadili mikakati na makubaliano na mkandarasi Salem Construction Limited ili kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wa Jengo la Taaluma unakamilika ifikapo Juni 2026.
Mradi huu, wenye thamani ya shilingi bilioni 13.5, unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa HEET chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Ujenzi wa jengo la ghorofa tatu unajumuisha madarasa ya kisasa, ofisi, na kumbi za mihadhara, likiwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 3,600 kwa wakati mmoja.
Prof. Pallangyo alisema: “Mradi huu ni zaidi ya jengo; ni uwekezaji wa kimkakati katika mustakabali wa elimu ya juu nchini Tanzania. Tunatarajia kuwa miundombinu hii itaimarisha uwezo wetu wa kutoa elimu bora na shindani kimataifa.”
Ujenzi huu unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa katika kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, na kuimarisha ubora wa elimu ya juu nchini.


