WAHITIMU 756 WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA UJASIRIAMALI NA TEKNOLOJIA

November 24, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma na Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu, Balozi Simon Sirro, amewatunuku vyeti wahitimu 756 wa Kampasi ya Kigoma na kuwatia moyo kuchangamkia fursa za uwekezaji na ujasiriamali. Balozi Sirro alisema kilimo cha kibiashara, utalii, biashara ndogo, ujasiriamali wa kidijitali, na huduma kwa jamii ni njia za kuunda miradi mipya na kuchangia maendeleo ya Kigoma.

Alisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia na akili bandia (AI) kuongeza ufanisi, kujifunza ujuzi wa kidijitali kama data analytics, e-commerce, digital marketing na cyber security, pamoja na kutumia mitandao ya kijamii kuunda fursa za biashara. Aliongeza kuwa waadilifu, wabunifu na walio tayari kubadilika ni muhimu kuunda ajira mpya na kuwa kizazi kipya cha viongozi wa kidijitali wenye maadili na ujasiri wa kujenga Tanzania ya kidijitali.

Sixbert Qamdiye, Mjumbe wa Bodi aliyewakilisha Wizara, alisema mafanikio ya vijana hutokana na bidii, uvumilivu na kujituma. Vijana wanapaswa kutumia ujuzi wa kidijitali, ubunifu wa teknolojia na AI kuboresha biashara, kuunda bidhaa na huduma mpya, kuongeza ushindani sokoni, na kubadilisha changamoto kuwa fursa. Kila mhitimu ana nafasi ya kuwa mjasiriamali wa kidijitali na kuchangia maendeleo ya uchumi wa kidijitali na viwanda, huku akidumisha maadili na uaminifu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa Pallangyo, alisema Mahafali ya Kwanza ya Kampasi ya Kigoma yanaashiria maendeleo makubwa. Kampasi mpya ya Kamala ina miundombinu ya kisasa inayoweza kuhudumia zaidi ya wanafunzi 1,700. TIA Kigoma ilianza mwaka 2014 na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 58 hadi karibu 1,000 mwaka wa masomo 2025/2026, ikionyesha mafanikio makubwa katika elimu ya ubunifu na ujasiriamali wa kidijitali.

Profesa Pallangyo pia alibainisha kuwa zaidi ya wanafunzi 517 wamefaulu mafunzo ya ujasiriamali kupitia JA-Digital, akiwataka wahitimu kuwa wabunifu wa suluhisho, si watumiaji tu wa teknolojia.

Mhitimu Jasmine Hamisi, Mwanafunzi Bora wa TIA ngazi ya Cheti cha Awali katika Fani ya Uhasibu kutoka Kigoma, alisema mafanikio yake yametokana na jitihada za kusoma bila kuchoka na kuweka malengo aliyoyajiegeta.

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/