WANAFUNZI 35 WA TIA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO CHUO KIKUU CHA MAKERERE, UGANDA

February 7, 2025

Jumla ya wanafunzi 35 wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wamefanya ziara ya mafunzo katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.

Ziara hii, iliyoanza tarehe 27 Januari 2025, inalenga kuwajengea uwezo wahadhiri, wanafunzi, na wafanyakazi waendeshaji katika nyanja za ubunifu, ujasiriamali, na vituo vya uatamizi wa biashara.

Mratibu wa ziara hiyo, ambaye pia ni Mkuu wa Sehemu ya Ukuzaji na Uendelezaji wa Wanafunzi Kitaaluma na Kitaalam, Mhadhiri Amani Matonya, amesema kuwa wanafunzi watajifunza mbinu za kukuza ubunifu wao, kushirikiana na wabunifu wenzao kutoka Uganda, na kujenga mtazamo wa kimkakati kuhusu maendeleo ya biashara.

“Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa mstari wa mbele kusisitiza umuhimu wa kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kuajirika. Katika kutekeleza dira hii, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Profesa William Amos Pallangyo, ameendelea kuhimiza juhudi za kuwaandaa vijana wa TIA kuingia katika soko la ajira la Afrika Mashariki na kuwahamasisha kuamini katika bunifu zao, ambazo zinaweza kuwa chachu ya mawazo ya kibiashara na kujiajiri,. alisema Mhadhiri Matonya.

Katika ziara hiyo, wanafunzi waliambatana na viongozi mbalimbali wa taasisi, wakiwemo Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi, Mkuu wa Sehemu ya Masomo ya Rasilimali Watu na Utawala, Afisa Masoko na Uhusiano, Afisa Usajili, pamoja na wahadhiri wanaoratibu maendeleo ya taaluma na kazi katika Kampasi za Kigoma na Mbeya.

Mbali na kujifunza kuhusu ujasiriamali na ubunifu, wanafunzi na wafanyakazi wa TIA pia wanatarajiwa kutembelea vivutio vya utalii nchini Uganda, shirika la Boundless Minds Organization, pamoja na maeneo mengine muhimu ya kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Ziara hii inatarajiwa kuleta matokeo chanya kwa washiriki, kuwahamasisha kuwa wabunifu, na kuwawezesha kutumia ujuzi walioupata kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla.

 

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/