WANACHUO WA TIA KAMPASI YA MWANZA WAPIKWA KWA ELIMU YA VITENDO

February 1, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mwanza imetoa mafunzo ya elimu kwa vitendo kwa kushirikiana na benki ya CRDB Jijini Mwanza.
Akifungua mafunzo hayo Mratibu wa Taaluma Kampasi ya Mwanza Ndg. Vicent Kuambiana ameishukuru CRDB kwa mafunzo hayo ambayo yataiwezesha TIA kutekeleza mtaala wa elimu kwa vitendo na hivyo kuwajengea wanachuo hao uwezo wa kujiajiri na kujiandaa katika soko la ajira.
Mafunzo hayo ambayo yalitolewa na Meneja Benki ya CRDB tawi la Buzuruga Ndg.Bakari Mshana yalilenga kuwafundisha wanachuo mahusiano ya fani zao za Uhasibu na Ugavi katika shughuli za benki na namna bora ya kutekeleza majukumu ya Uhasibu na Ununuzi na Ugavi.
Meneja Bakari amesema ni muhimu ukiwa mwanachuo kujua kwa vitendo kuhusu fani  unayosomea ili uweze kutekeleza majukumu kwa ufasaha ukijiajiriwa na ukijiajiri.
“Mimi ni mhitimu wa TIA mwaka 2007 ambaye naishukuru sana TIA kwa kunipatia elimu iliyonifanya niweze kuaminiwa na Benki hii kubwa nchini inayotanguliza mbele maslahi ya wananchi, haya ni matunda mazuri ya elimu ya Taasisi hii,”. Alisema Meneja Bakari
Taasisi ya Uhasibu Tanzania inaendelea kuhakikisha Wanachuo wanapata elimu yenye ufanisi kwa kuwaunganisha na wanataaluma ambao wapo katika soko la ajira lakini pia ambao tayari wamejiajiri ili kutoa wanachuo ambao sio tegemezi katika jamii.
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/