TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

WAHITIMU WA TIA WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUSOMA VITABU

November 30, 2022
Mkuu wa Mkoa wa  Singida Mhe.Peter Serukamba amewaasa Wahitimu  3,666 kujenga utamaduni wa kusoma vitabu  ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia katika kada husika, maarifa mengi yameficha kwenye vitabu hivyo.
Mhe. Serukamba amesema teknolojia inabadilika kila siku, ili kuendana na kasi ya hiyo na ushindani wa ajira na kujiajiri ni muhimu kwa Mhitimu kusoma vitabu mara kwa mara hususani vya matoleo mapya ya
“Mfano Wahasibu kila siku mifumo inaongezeka na kubadilika, kupitia vitabu matoleo ya sasa itawaongezea utaalamu zaidi na kujiandaa kuwa tayari kupokea mabadiliko hayo ya kidigitali,”. Alisema RC Serukamba
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Serukamba amesema hayo akiwatunuku wahitimu hao katika Mahafali ya 20 na ya 11 kufanyika kampasi ya Singida yakijumuisha Wahitimu kutoka Kampasi ya Mwanza, Kigoma na Singida yenyewe akiwa mgeni rasmi aliyemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mwingulu Nchemba (MB).
Aidha, Mhe.Serukamba ameipongeza  TIA kwa hatua ya kubwa ya kuanzisha Vituo atamizi ( Incubation Centres) ambavyo vitawaandaa wanachuo wahitimu kujiajiri kwa kulea na kuendeleza wazo mradi aliloanzisha Mwanachuo huyo.
“Mefurahi kuona wanachuo leo wameonesha uthubutu na kufanyia kazi mawazo yao na ubunifu wao katika kujiajiri huku wakisoma, na wengine mapato wanayopata kwenye kujiajiri kwao wanajikimu na kulipa ada,”. Alisema Mhe. Serukamba
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/