Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael amewataka Wakuu wa Taasisi za Elimu ya juu kuendelea kupokea ushauri unaotolewa na TCU na kuutekeleza pamoja na kushiriki maonesho hayo kwa kuwa yanaziwezesha Taasisi za Elimu ya Juu kukutana na wadau moja kwa moja.
Amesema hayo wakati akihitimisha Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ya leo tarehe 23/7/2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
Pia Dkt. Michael ameviasa Vyuo kuzingatia sheria na kanuni kwa kufuata mwongozo na taratibu wakati udahili.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania ni moja kati ya Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyoshiriki maonesho hayo na kuwatunuku cheti cha ushiriki.