TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

VITUO ATAMIZI KUANZISHWA TIA

November 16, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu  wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William Pallangyo amesema ili kuimarisha na kuendeleza ari ya ujasiriamali, TIA imejipanga kufungua vituo atamizi (incubation centres) ambapo wazo mradi la Mwanachuo litalelewa na kuendelezwa, na  kuunganishwa na taasisi mbalimbali kulingana na aina ya mradi zikiwemo taasisi za kifedha.

Aidha, Profesa Pallangyo amesema katika kuhakikisha tunawaandaa Wanachuo kukua kiujuzi na kitaaluma, TIA Kampasi ya Mbeya imewapa fursa wanachuo kujifunza kwa vitendo na kuunga mkono juhudi zao katika mawazo yao ya biashara na uwekezaji.

“Wanachuo waliojiunga na kuanzisha biashara zao wameongezeka na biashara zao zinazidi kukua kama ambavyo umeshuhudia ulipotembelea banda la maonesho,”.  Amesema Profesa Pallangyo

Pia Profesa Pallangyo ameongeza kuwa jitihada hizi ni kuendelea kuunga mkono juhudi  za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kukuza mawazo ya biashara ya vijana wabunifu kwa  maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Amesema hayo katika mahafali ya 20 na ya 10 kufanyika Kampasi ya Mbeya ambapo jumla ya Wahitimu wa Mwaka 2021/2022 kwa kampasi zote (Dar es Salaam, Mbeya, Singida, Mtwara, Mwanza na Kigoma) ni 13,595 ambapo Wanawake 7,154 sawa na asilimia 52.6 na Wanaume 6,441 sawa na asilimia 47.4,

“Hivyo, Wahitimu hawa wa leo wa Kampasi ya Mbeya ni asilimia 17.3 ya wahitimu wote wa Taasisi kwa mwaka 2021/22,”. Amesema Profesa Pallangyo

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/