TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

“UKOMO WA ELIMU UTATEGEMEA MAARIFA ULIYONAYO ” WAKILI MUSENDO

November 16, 2022
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Chiguma Musendo amesema elimu haina mwisho ila ukomo wake utategemea na maarifa uliyonayo, kuna watu hawakusoma na waliweza kuvumbua vitu kurahisisha maisha yao, Soko la ajira haliangalii gharama za elimu uliyotumia, bali huangalia maarifa na stadi kazi zitokanazo na elimu.

“Maarifa huzalisha mbinu za kazi (skills), ili uwe bora sana kwenye kila unalolifanya basi wekeza kwenye elimu, lakini ili ufanikiwe ishi kwenye maarifa,”. Amesema Wakili Musendo

Wakili Musendo amesema bodi hii ina furaha kubwa zaidi kwa sababu miongoni mwa wahitimu wa leo walianzia ngazi ya cheti cha awali Bodi ikiwepo, na sasa wanapata Shahada bodi ikishuhudia,

“kwa kipindi hicho kuanzia Mwaka wa Masomo 2017/2018 kumekuwapo na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwa kiwango cha asilimia 46.5 kutoka 14,918 hadi kufikia wanafunzi 21,856 mwaka 2020/2021,”. Amesema Wakili Musendo

Katika hotuba yake Wakili Musendo amewapongeza Wahitimu kwa kuruka viunzi mbalimbali vya kitaaaluma na kijamii na kuweza kupata vyeti kama ushahidi wa viwango vyao vya elimu na kuwaasa kujiendeleza kwenye fani zao na fani nyingine ili kuendana na mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia na kidijitali.

Pia Wakili Musendo amesema  Bodi inampongeza rasmi Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William Amos Pallangyo kwa kuteuliwa kuiongoza Taasisi hii kongwe yenye fani mbalimbali zilizobobea kwenye uchumi na biashara.

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/