UJENZI WA KAMPASI MPYA YA TIA  MWANZA UNAENDELEA

March 22, 2022
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt.Momole Kasambala pamoja na Meneja wa TIA Mwanza Dkt.Honest Kimario wametembelea Ujenzi wa Kampasi mpya unaoendelea
Nyang’homango, wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza leo tarehe 21/03/2022.
Mradi huo ambao unaofadhiliwa na Serikali chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ambao utagharimu B. 7.8 unatarajiwa kukamilika mapema 2024.
Aidha, Ujenzi wa Kampasi hiyo utakuwa ni fursa kwa wakazi  wa maeneo ya Mwanza,Mara, Geita na Mikoa mingine jirani.
Dkt. Kimario Meneja wa Kampasi ya Mwanza amesema. ” baada ya kukamilika kwa mradi huo TIA itaweza kuhudumia Wanachuo 1,550 kwa wakati mmoja, Ujenzi huo utajumuisha Jengo la Maktaba lenye uwezo wa kuhudumia Wanachuo 250, Maabara ya Kisasa ya Kompyuta yenye uwezo wa kudumia Wanachuo 200,.Amesema Dkt. Kimario.
Pia, Dkt Kimario ametoa wito kwa wakazi kanda ya Ziwa kujiandaa kwa kuwa miundombinu ya kusomea na kufundishia iboreshwa zaidi na ili kuendelea kutoa elimu yenye ufanisi.  Ni wakati sasa vijana wa Kanda ya Ziwa kutumia fursa hii kwa  kuwa TIA ina mazingira rafiki ya kusomea na kufundishia.
TIA inaendelea  kuboresha miundombinu katika Kampasi zake tatu za mikakati ambazo ni Mtwara, Kigoma pamoja na Mwanza yenyewe.
TIA Kazi inaendelea kwa kasi.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/