Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William A. Pallangyo leo ametembelea  maonesho ya Mafunzo ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) yanayoendelea katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma.
Profesa Pallangyo amesema TIA tuendelee kutangaza majukumu makuu ya Taasisi kwa Umma, kwenye nyanja bobezi za Mafunzo,Tafuti na Ushauri ili kuwa na Wanafunzi bora watakaopata elimu yenye Ufanisi itakayowaandaa kujiajiri na kuajiriwa
“Leo kwenye maonesho haya mefurahi kumuona Kijana wa TIA kutoka Kampasi ya Mbeya Gift Lutumo ambaye ni Mkulima, tena katika umri mdogo na anatoa elimu ya Parachichi kwenye banda letu ambayo ina Soko kubwa Marekani, hili ni la kujivunia sana,”. Alisema Profesa Pallangyo
Taasisi ya Uhasibu Tanzania inakukaribisha katika Banda lake Viwanja vya Jamhuri  geti la Nyuma upande wa kushoto kwenye kona ya Goli la mwisho.
Katika Banda hili utapata huduma za Udahili kama Kozi zinazotolewa,ushauri wa kozi za kusoma kulingana na ufaulu wa Mwanafunzi kuanzia ngazi ya cheti cha awali, Stashahada, Shahada ya Kwanza, Stashahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamili, pia utapata huduma za Utafiti na Ushauri wa kitaalam.





