TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WASTAAFU WATARAJIWA WA TRA

December 14, 2022

Taasisi ya Uhasibu Tanzani (TIA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaendesha mafunzo ya maisha baada ya kustaafu kwa watumishi wastaafu watarajiwa takribani 110 kwa wiki moja kuanzia tarehe 12 mpaka 16, disemba 2022 katika Ukumbi wa New Savoi Mkoani Morogoro.

Akifungua mafunzo hayo, Godwin Barongo John, Meneja Kanda TRA Morogoro ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala amesema wameamua kufanya mafunzo hayo ili kuwaandaa watumishi wanaotarajia kustaafu kukabiliana na changamoto pindi watakapomaliza kuhudumu katika taasisi hiyo,

“Ili kuhakikisha Wastaafu wetu wanapata mafunzo yenye uhalisia wa maisha baada ya kustaafu, tumechagua Taasisi ya Uhasibu Tanzania kutoa elimu hiyo kwani ni wabobezi wa eneo hilo wakiwa na tafiti ya maisha wanaoishi watumishi wastaafu,”. Amesema Meneja Godwin

Mwenzeshaji Dkt. Issaya Hassanal ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Fedha na Utawala amesema ni muhimu kujiandaa mapema kabla ya kustaafu ili kuepuka kuishi maisha yatakayokupa msongo wa mawazo

“Ukistaafu maisha hubadilika kwa mtumishi, familia yake, majirani na hata eneo ulilokuwa unafanyia kazi, TIA inatoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo kwa namna bora ya kutengeneza mpango wa biashara na kuendeleza iliyopo na Mtindo bora wa maisha ,”. Amesema Dkt.Hassanal

Naye Mwenzeshaji Dkt. Abdallah Gorah ambaye ni Mkuu wa Idara ya Tafiti na Ushauri amesema Wastaafu wengi wamekua wakiishi maisha duni sana pindi wanapomaliza kuhudumu kwasababu ya kutokuwa na matumizi mazuri ya muda na bajeti.

Bi.Prisca Kisaka Mtumishi wa TRA amesema amefurahia sana mafunzo haya yenye ufanisi mkubwa kutoka Taasisi y Uhasibu Tanzania na ameishukuru Taasisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mafunzo haya ambayo yanawaandaa vyema kukabiliana na maisha baada ya kustaafu.

Mratibu wa mafunzo kutoka TIA Bi. Dorah Chenyambuga ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi amesema Taasisi ya Uhasibu Tanzania imeendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wa Umma katika nyanja mbalimbali ikiwa ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi na maisha baada ya kustaafu.

 

 

 

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/