Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) lmendesha Mafunzo kwa Watumishi wake ya kujiandaa kustaafu.Mafunzo haya yatawawezesha Watumishi hao kukabiliana na changamoto baada ya kikomo cha Utumishi wa Umma.
Wakati akifungua Mafunzo hayo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Dkt Momole Kasambala amesisitiza ” ni muhimu kuanza kuwekeza mapema pale tu unapoanza ajira yako kwa kuwa na miradi itakayokuingizia kipato cha kila siku ili pindi utakapostaff uwe umejipanga”,. Alisema Dkt.Kasambala.
Mafunzo hayo ya siku tano ambayo yameanza leo tarehe 21 – 26/03/2022 yanafanyika Ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza