Taasisi ya Uhasibu Tanzania imeanza kutoa Mafunzo kwa Miaka Mitatu mfululizo kwa Wastaafu watarajiwa kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ili kuwajengea uwezo wa kujiandaa mapema kuelekea kikomo cha Utumishi wa Umma.
Akifungua Mafunzo hayo Prof.James Mdoe Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa kuendelea kuwa vinara wazuri na wa kuaminika katika yaliyozingatia tafiti na Ushauri mbalimbali hivyo kuwa taasisi yenye ubora na weledi mkubwa.
Mafunzo hayo yanayoendelea katika Chuo Cha Ualimu Morogoro ukumbi wa Franken na Wawezashaji kutoka TIA wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Fedha,Mipango na Utawala Dkt.Isaya Hassanal pamoja na Idara ya Utafiti na Ushauri wakiongozwa na Dkt.Abdallah Gorah yamelenga kuwaandaa Wastaafu watarajiwa zaidi ya 200 kukabiliana na changamoto zitakazojidhihirisha kiafya,kiuchumi na kimazingira baada ya kumaliza kuhudumu Utumishi yani kuwapa nguvu ya kudhamiria kupata wanachofanya kwa mikono yao, bila kutegemea watu wengine.
TIA imelenga kuwaandaa Wastaafu watarajiwa kukabiliana na changamoto zitakazojidhihirisha kiafya,kiuchumi na kimazingira baada ya kumaliza kuhudumu Utumishi yani kuwapa nguvu ya kudhamiria kupata wanachofanya kwa mikono yao, bila kutegemea watu wengine.
Aidha, Mafunzo hayo yamejikita Kuwajengea Wastaafu Mazingira wezeshi ili kupata Mafao yao na kuyatumia kwa tija.
Pia kuhakikisha wastaafu watarajiwa wanafahamu haki zao za msingi na vitu gani muhimu watahitajika kuwa navyo katika kipindi cha Kujiandaa kustaafu.
*”Sistaafu Maisha,nastaafu kazi”*. Dkt.Mkumbo