TIA YASISITIZWA KUENDELEA KUFANYA TAFITI KWA MAENDELEO YA UCHUMI NA BIASHARA 

November 12, 2024
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), imeandaa Kongamano la tatu (3) la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Ukuaji wa Uchumi linaloendelea jijini Arusha, ambalo limeanza jana tarehe 7 hadi 9 Novemba, 2024.
 Kongamano hilo limehusisha watafiti, wataaluma, Wadau wote wa uchumi na Biashara toka ndani na nje ya nchi.
 Wakati akifungua Kongamano hilo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu, Mhe Doto Biteko, (MB) amesema watafiti wanatakiwa kufanya tafiti zenye tija na kutoa matokeo ya tafiti zao ili ziwanufaishe wananchi katika kuhakikikisha changamoto za jamii zinatatuliwa sambamba na kukuza uchumi.
 Naye, Naibu Waziri wa Viwanda na  Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (MB) amesema ni wakati muafaka wa tafiti zinazotolewa na wataalamu hao kuanza kuzitumia kudadavua kwa kina juu ya mwelekeo wa uchumi haswa katika ubunifu wa biashara na uchumi hususani katika tafiti atamizi.
 Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya  Ushauri ya Wizara, Profesa Jehovaness Aikael  amesema watafiti lazima kuendelea kufanya tafiti zaidi katika uwekezaji, usimamizi wa biashara ndani na nje ya nchi ili kuimarisha uchumi na uboreshaji mazingira ya biashara na kufikia malengo ya milenia.
 Pia Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Profesa William Pallangyo amesema TIA itaendelea kufanya tafiti ambazo zinagusa jamii na taifa kwa ujumla hususani tafiti zinazogusa maendeleo ya uchumi na biashara katika uwekezaji.
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/