TIA YASHIRIKI NANE NANE KATIKA MIKOA MITATU

August 9, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania inashiriki katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa Mbeya, Kanda ya Ziwa Mwanza na Kanda ya Kaskazini Arusha ikiwa na Kauli mbiu ” Agenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Dkt.Momole Kasambala Makamu Mkuu wa Chuo upande wa Taaluma, Tafiti na Ushauri ambaye amemuwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu amesema TIA inajukumu kubwa sana la kuwawezesha na kuwajengea uwezo  Wanafunzi wetu katika kuanzisha wazo la biashara na kuwa wabunifu katika fani walizobobea.
Aidha, TIA inatekeleza elimu kwa vitendo kwa kutoa ushauri na mafunzo ya utunzaji wa kumbukumbu za Biashara, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Nidhamu ya Fedha, Kutambua fursa na kuandaa mpango biashara.
Pia inafanya tafiti na kutoa ushauri wa Kitaalam unaoziwezesha Taasisi za Umma ikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa kutathmini na kuibua vyanzo vya mapato.
Maonesho haya ya Nane Nane yamefunguliwa rasmi Kitaifa Jijini Mbeya, yatakayodumu kwa siku 8 kuanzia tarehe 1 hadi 8, 2022.
Karibu utembelee mabanda yetu upate huduma bora yenye ufanisi kwa maendeleo ya Taifa letu.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/