TIA YASHIRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA RASILIMALI WATU

May 19, 2022
Arusha
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo imeshiriki na kuwa moja ya wadhamini wa Kongamano la Kimataifa la Rasilimali Watu linalofanyika  Jijini Arusha kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 18 hadi tarehe 20 Mei, 2022 ambalo limelenga kuwakutanisha Wataalamu wa Kada ya Rasilimali Watu katika kikao kazi cha kuboresha Taaluma yao.
Naye, Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi ya TIA Fedha na Utawala Dkt.Issaya Hassanal amepata fursa ya kutoa mada ya  maadili ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ikiwa ni kuwakumbusha zaidi kwani ndiyo wasimamizi wakuu wa maadili mahali pa kazi.
Kupitia kongamo hili, TIA imeweza kutangaza huduma mbalimbali zinazotolewa katika Taasisi hiyo hususani Programu za muda mrefu ambazo ni Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma.
TIA imekuwa mdau mkubwa wa kada ya Rasilimali Watu kwani kwa sasa imeanzisha Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Rasilimali Watu na Teknolojia ya Habari, kuanzishwa kwa programu hii ambayo inaendana na mabadiliko ya Teknolojia itasaidia Maafisa Rasilimali Watu kuwa wa kidigitali zaidi.
Na pia TIA inatoa programu za muda mfupi ambazo zimejikita katika  masuala ya Uhasibu, Rasilimali Watu na Utawala, Huduma kwa Mteja, Ukusanyaji na Usimamizi wa Fedha za Umma pamoja na Mafunzo ya kujiandaa kustaafu.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/