Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman atoa tuzo kwa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Mhe.Haroun Ali Suleiman amekabidhi tuzo hiyo ya shukrani leo tarehe 20/05/2022 katika Kongamano la Rasilimali Watu ikiwa ni Kilele cha Siku ya Kimataifa ya Rasilimali Watu kilichofanyika Jijini Arusha Ukumbi wa Mount Meru.
Tuzo hiyo imepokelewa na Mratibu wa Mafunzo Bi.Dorah chenyambuga kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA.
Chuo cha TIA ni mdau mkubwa katika kutoa Mafunzo ya Rasilimali Watu sambamba na nyanja nyingine za Uhasibu, Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Masoko na Uhusiano, Uhasibu wa Umma na Fedha ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada Stashahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamilii.