TIA YAJIVUNIA VIJANA 3 WAZALENDO NA JASIRI

June 29, 2022
Afisa Mtendaji Mkuu Profesa Pallangyo leo amewapongeza Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania waliotunukiwa vyeti pamoja na Nishani ya Heshima na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha uzalendo na ujasiri na kuvunja rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku 3 tu badala ya siku 6 kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengine wanaopanda mlima huo.
Wanachuo hao wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania  Innocent George Masanja anayesoma Shahada ya Uongozi wa Rasilimali watu na Fadhili Jonathan Naaman anayesoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara wamepanda Mlima Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru ya mwaka huu 2022.
Sambamba na hilo, Pia Skauti Taifa wametoa shukrani kwa TIA  kupitia  Afisa Mtendaji Mkuu Profesa William Pallangyo na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt. Momole Kasambala kwa kuwatunuku vyeti vya Shukrani kwa kuwawezesha kuandika historia hiyo kubwa kwao na Taifa kwa ujumla.
Tukio hili la kihistoria limeipeperusha bendera ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kitaifa na Kimataifa, na hakika TIA inajivunia kuwa na vijana Shupavu, Jasiri na wachapakazi.
                 
                
                
                
                
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/