TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA WATAKIWA KUFANYA KAZI NA JAMII

September 15, 2022

Mbeya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amesema Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ina jukumu kubwa la kufanya tafiti katika jamii ili kubaini changamoto zinazowakibili na kutoa mkakati wa kutatua changamoto hizo na kuisaidia Serikali.

“TIA fanyeni kazi na jamii kujua changamoto zao na kuja na mkakati madhubuti ya kutatua changamoto hizo, ili kusaidia Serikali,”.  Alisema Dkt. Mpango

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango alipotembelea banda la TIA katika Mkutano Mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania – ALAT, wenye Kauli Mbiu; “Kuongeza Tija katika Ukusanyaji na Matumizi bora ya Mapato kwa Halmashauri ni Msingi wa Maendeleo endelevu kwa Wananchi” uliofanyika katika ukumbi wa Eden-Highlands hotel Jijini Mbeya.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai Dionis Myinga ambaye ni mmoja wa washiriki wa mkutano huo ameipongeza Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa kuendelea kutoa mafunzo na kufanya tafiti kwa Halmashauri ambazo zinahudumia jamii moja kwa moja na zenye uhitaji wa kubuni na kuongeza vyanzo vya mapato ili kuendelea kutoa huduma bora na kuendeleza maendeleo ya miundombinu ya afya na elimu.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) inatoa mafunzo na kufanya tafiti zinazogusa maisha ya Jamii katika nyanja za uhasibu, uchumi, biashara, ujasiliamali, ugavi na ununuzi na kutoa mafunzo ya uibuaji vyanzo vya mapato na matumizi sahihi ya mapato kwa Serikali za Mitaa.

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/