TIA WAPEWA MAFUNZO YA SHERIA ZA UNUNUZI.

March 29, 2022
Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania wanapatiwa Mafunzo ya Sheria ya Ununuzi  wa Umma, Sura ya 410 pamoja na marekebisho yake, ili kuongeza ufanisi katika kuzingatia taratibu, sheria na kanuni za manunuzi.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na wawezeshaji kutoka Mamlaka ya kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa muda wa siku 4 kuanzia leo tarehe 29/03- 01/04/2022 katika Ukumbi wa Veta Jijini Tanga.
Pia, wawezeshaji wametambulisha mfumo wa mafunzo uitwao tsms.ppra.go.tz ambao washiriki wanaweza kujisajili na kupata taarifa mbalimbali juu ya Manunuzi na Ugavi ikiwa ni sehemu ya mafunzo.
Wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Dkt.Momole Kasambala amesema “Mafunzo haya yatawawezesha kwenda kuboresha utendaji wa kazi na kuongeza uelewa wa kusimamia manunuzi yenye uwazi na ukweli, hivyo yawapasa kuzingatia masomo kwa kuwa ni muhimu kwa Taasisi yetu kwani sasa tuko katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo,”. Amesema Dkt.Kasambala.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania itaendelea kujikita katika kuzingatia kufanya manunuzi ambayo yanaendana na taratibu na sheria za Ununuzi.
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/