Afisa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William A. Pallangyo akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Moses Dulle wametembelea mradi wa ujenzi Kampasi ya Mwanza katika eneo la Nyang’homango Misungwi jijini Mwanza.
Mradi huo unaohusisha ujenzi wa Jengo la Taaluma lenye madarasa 9 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1100, jengo la utawala lenye ofisi 16, Maabara ya kisasa ya Kompyuta yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 200 pamoja na Maktaba kubwa ya kutumiwa na wanafunzi 250 kwa wakati mmoja, kukamilika kwa majengo hayo kutaongeza udahili na kurahisisha mazingira wezeshi ya kusomea na kufundishia.
Ujenzi wa mradi huu unathamani ya shilingi za kitanzania bil 7.8 fedha ambazo TIA imefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.
Katika ziara hiyo pia waliambatana na Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala TIA – Dkt. Issaya Hassanali, pamoja na Maafisa waandamizi kutoka TIA na Wizara ya Fedha na Mipango.





