Fainali ya mashindano ya Madarasa yamefanyika leo kwa Wanachuo wa TIA katika viwanja vya Uhasibu Kurasini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Dkt.Issaya Hassanal, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi na kutoa zawadi kwa washindi.
Awali wakati akifungua mashindano hayo Dkt. Hassanal aliwataka Wanachuo kuchukulia mashindano ya michezo hiyo kama chachu ya kukuza vipaji vyao lakini pia kujenga mahusiano mema na ushirikiano mzuri baina ya wanachuo, na kuwasisitiza kucheza kwa amani na upendo.
Katika mchezo wa Fainali, Wanachuo wa mwaka wa pili waibuka mabingwa dhidi ya mwaka wa tatu katika mpira wa miguu kwa Goli 1 kwa 0.
Upande wa mpira wa pete Wanachuo wa Cheti na Diploma waibuka kidedea dhidi ya Wanachuo wa Shahada ya Kwanza mwaka wa pili na wa tatu kwa kuwachabanga magoli 60 kwa 56.
Nao wakali wa mpira wa wavu, wanachuo wa mwaka wa kwanza na diploma waliwabamiza seti 3 dhidi ya seti 1 wanachuo wenzao wa mwaka wa kwanza na diploma.
Huku Wanawake nao wakiwakilisha vyema kwenye mpira wa pete, kwa mpambano mkali ambapo mwaka wa kwanza waibuka washindi dhidi ya mwaka wa tatu kwa magoli 56 kwa 43.
Mashindano haya ni maandalizi ya mashindano ya vyuo vikuu SHIMIVUTA.