TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA KUANZA MATUMIZI YA MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO e-MREJESHO

March 19, 2022
Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo, wameanza Mafunzo ya Mfumo wa e-Mrejesho yatakayodumu kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 18 – 22/03/2022 katika Kampasi ya Singida.
Mfumo huu wa e- mrejesho utawezesha kushughulikia malalamiko kwa usiri na mrejesho wa haraka.
Mafunzo haya yameendeshwa  na Ofisi ya Rais Menejimenti  ya Utumishi wa Umma na Utawala bora (OR- MUUUB).
Kupitia mfumo huu, Wananchi (Wanachuo)) wataweza kufungua akaunti kwenye mfumo na kutoa malalamiko, kufuatilia lalamiko hilo na kupata mrejesho kupitia akaunti yake hiyo kwenye tovuti au kwa programu ya simu ya mkononi “Mobile App”.
 
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifuatilia mada mbalimbali
zilizo wasilishwa sambamba na mafunzo ya mfumo wa e-Mrejesho
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/