Taasisi ya Uhasibu Tanzania imeendelea kwa kasi ya “Kazi Iendelee” katika kuhakikisha inatoa elimu yenye ufanisi kwa uboreshaji wa miundombinu.
Leo, TIA imesaini Mkataba na mkandarasi kampuni ya Masasi Construction katika ujenzi wa Maabara ya Kompyuta, Maktaba na Ukumbi wa Mihadhara wa Kampasi ya Mbeya.
Mradi huo ambao unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 09/03/2022 baada ya mkandarasi huyo kukabidhiwa “site” ili kuanza ujenzi.
Ujenzi wa mradi huu utagharimu kiasi cha tshs.Bilioni 3.3 na unatarajiwa kukamilika ndani ya wiki 20.