TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA KAMPASI YA SINGIDA YASHIRIKI UZINDUZI WA UPANDAJI MITI

February 1, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeshiriki uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti mkoani Singida, zoezi ambalo limeendeshwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe.Mhandisi Paskaz Muragili kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Dkt.Binilith Mahenge.
Katika Uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya alisema mazingira ni uhai na utunzaji wake ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha, alitoa rai kwa wananchi kuweka mazingira safi kwa kutupa taka sehemu husika zilizoandaliwa ili kuweka mji safi, kupanda miti ya kila aina katika makazi yao na kupanda mazao ya muda mfupi yenye kustahimili ukame.
                               
Katika kuunga  mkono jitihada za Serikali kwenye utunzaji wa mazingira, Meneja Kampasi ya Singida Dkt.James Mrema aliwaongoza Wafanyakazi wa TIA katika zoezi la upandaji miti ili kwa pamoja kuifanya Singida ya Kijani na kuboresha mazingira rafiki kwa Wanachuo wa Kampasi hiyo.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania, Elimu kwa ufanisi.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/