TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

TIA KAMPASI YA KIGOMA YAWANOA WAFANYAKAZI WA CAMBRIGESHIRE ACADEMY

February 1, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Kigoma imetoa mafunzo kwa Wafanyakazi ya Shule ya Cambrigeshire Academy iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Mafunzo hayo yalilenga kuboresha utendaji wa Taasisi ya Cambridge hususani katika nyanja za utoaji huduma kwa wateja, utafutaji wa masoko, Sheria za biashara na kazi, usimamizi wa Bohari na ununuzi pamoja na utunzaji wa fedha ambayo yaliendeshwa na wawezeshaji wabobezi 10 kwa siku 5 kutoka TIA kampasi ya Kigoma.
Aidha, mafunzo hayo yamewajengea uwezo wafanyakazi wa shule ya Cambrigeshire Academy ili kuboresha  mazingira ya Wanafunzi kupata elimu bora.
TIA imeendelea kuwa kinara wa utoaji mafunzo katika kuboresha huduma zitolewazo katika Taasisi mbalimbali kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/