Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Prof. William A.Pallangyo amemkabidhi gari  Kaimu Meneja wa Kampasi ya Kigoma Mhadhiri Martin Mnyili, leo katika Kampasi ya Singida.
Wakati akimkabidhi gari hilo, Prof.Pallangyo amesisitiza utunzaji wa magari hayo kwani yananunuliwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Taasisi.
Naye, Mhadhiri Martin Mnyili ameishukuru Taasisi kwa kumpatia kitendea kazi muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kampasi ya Kigoma na kuahidi kuitunza vyema.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na baadhi ya viongozi ambao wapo SINGIDA kwa kazi maalum za Taasisi pamoja na Wafanyakazi wengine wa TIA.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya utoaji huduma ya kufundishia na kusomea Ili kuendelea kutoa elimu yenye ufanisi.