Taasisi ya Uhasibu Tanzania chini ya uongozi wa Dkt.Momole Kasambala Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu imedhamiria kuboresha Miundombinu ya kusomea na kufundishia ili kuendelea kutoa elimu yenye ufanisi.
Katika kuhakikisha dhamira hiyo inatimia TIA imeanza miradi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali Kampasi ya Mtwara ambapo jengo la Maktaba na Maabara ya Kompyuta pamoja na Madarasa ujenzi umefikia hatua ya kumwanga sakafu ya mwisho kabla ya kupaua.
Jengo la Maktaba na Maabara ya Kompyuta katka hatua ya Sakafu ya mwisho kabla ya kupaua.
Jengo la Madarasa upande wa mbele.