TAASISI YA TIA YAPONGEZWA KWA KUWA NA BARAZA IMARA LA WAFANYAKAZI

February 22, 2022
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Hamad Hassan Chande ameipongeza Taasisi ya TIA kwa kuwa na Baraza imara la Wafanyakazi ambapo wawakilishi wa Wafanyakazi hao wamechaguliwa kwa demokrasia.
Mhe. Hamad Hassan amesema hayo leo, alipokuwa akifungua kikao cha Baraza Kuu la Nne la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania kilichofanyika Kampasi ya TIA Singida ambapo ameongeza kuwa mabaraza hayo ni chombo muhimu cha kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi.
Mhe. Chande amesema Serikali inazingatia suala la Taasisi zake kuwa na mabaraza ya Wafanyakazi kwa kuwa mabaraza haya yanaanzishwa kisheria kwa madhumuni ya kuwashirikisha watumishi katika kujadili na kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu ajira ili kuongeza tija.
“Taasisi ambayo hakuna ushirikiano baina ya mwajiri na watumishi ni vigumu kutimiza malengo yake hata kama kutakuwa na Sera, Sheria na Kanuni nzuri Mahali pa kazi.”, amesisitiza Mhe. Chande.
Aidha, Mhe.Chande ametoa rai kwa Mkoa wa Singida kutumia Taasisi ya Uhasibu Tanzania katika Tafiti mbalimbali za Mkoa huo kwa maslahi ya Taifa na kuwa suluhu ya matatizo yanayotokea katika Jamii.
“Niendelee kuwasisitiza kuongeza juhudi katika maeneo ya Tafiti na huduma za Ushauri, hapa tafiti ndizo zinaleta “Legacy” ya Nchi na suluhu za Maslahi ya Taifa, ushindani wa “East Africa” wa vyuo vilivyoshauri Serikali zao TIA iwepo moja wapo, ni matarajio kwamba wataalamu wetu wataanza kwa kasi,”. amesema Mhe. Chande
Pia Mhe. Chande ameiagiza TIA kuanzisha kozi ya “Monitoring na Evaluation” kwakuwa  Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ambayo inahitaji ufuatiliaji na tathimini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania ni miongoni mwa Taasisi kongwe za elimu ya juu nchini yenye Kampasi 6 katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,
Mtwara, Singida, Mwanza, Kigoma  na Makao Makuu Dar es Salaam.
      
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/