PROF. PALLANGYO AFANYA KIKAO KAZI NA WAFANYAKAZI 

June 29, 2022
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William Pallangyo amefanya kikao kazi na Wafanyakazi wa TIA kampasi ya Dar es Salaam, leo Ukumbi wa Mihadhara ikiwa ni Mara ya kwanza  tangu alipoteuliwa katika nafasi hiyo.
Katika kikao hiko, Profesa Pallangyo amesisitiza wafanyakazi kufuatilia dhima na dhamira ya Taasisi pamoja na kuzingatia imani ya msingi ambayo itafanya tuweze kutoa huduma bora kwa wateja na kuwa wawabikaji.
Aidha Profesa Pallangyo amewaasa Wafanyakazi  kuzingatia sheria taratibu za utumishi wa umma kwa kuboresha utendaji wa kazi na kufanya kazi kwa weledi.
Pia Profesa Pallangyo amepokea maoni na michango kutoka kwa Wafanyakazi sambasamba na kutolea ufafanuzi wa kina kuhusu mambo yaliyowasilishwa katika kikao hiko.
Profesa Pallangyo amesema TIA ipo mbioni kuanzisha kozi za Shahada ya Uzamili Jijini Dodoma na Visiwani Zanzibar,
“TIA inazidi Kukua hivyo ni wajibu wa kila mmoja  ambaye ni mfanyakazi kuwa balozi wa kuisemea vizuri TIA,”. Alisisitiza Profesa Pallangyo
Taasisi ya Uhasibu Tanzania inatoa huduma ya mafunzo, kutoa ushauri na tafiti katika nyanja za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi pamoja na maeneo mengine ya biashara.
1
2
Pichani 1A na 1B hapo juu, aliyesimama katikati ni Prof. William A. Palangyo, Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022.
3
4
5
6
7
Picha 3 – 7 hapo juu, ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. William A. Palangyo, kwenye kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022
.    
8
9
10
11
12
Picha 8 – 12 hapo juu, ni baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakitoa hoja ama kuuliza maswali kwenye kikao kazi kati ya Mkuu wa Taasisi Prof. William A. Palangyo na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Taasisi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022
Pichani ni uongozi wa juu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ambapo aliyekaa katikati ni Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. William A. Palangyo, kushoto ni makamu mkuu wa Taasisi anayeshughulikia Taaluma Dkt. Momole Kasambala na kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi anayeshughulikia Mipango na Utawala Dkt. Isaya Hassanali wakifuatilia maswali na hoja za wafanyakazi  kwenye kikao kazi kati ya wafanyakazi wa TIA Makao Makuu na Mkuu wa Taasisi hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022
Pichani ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) anayeshughulikia taaluma Dkt. Momole Kasambala akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja na kujinu maswali ya wafanyakazi  kwenye kikao kazi kati ya wafanyakazi wa TIA Makao Makuu na Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. William A. Palangyo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022
Pichani ni Dkt. Modest Assenga akitoa nukuu ya mambo muhimu aliyozungumza Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) pamoja na hoja za wafanyakazi  kwenye kikao kazi kati ya wafanyakazi wa TIA Makao Makuu na Mkuu wa Taasisi hiyo Prof. William A. Palangyo, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Taaluma Jijini Dare es Salaam, Juni 28, 2022
Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/