Prof.Pallangyo atembelea Kampasi ya Singida

May 22, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William A. Pallangyo ametembelea Kampasi ya Singida akifuatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri Dkt. Momole Kasambala, Meneja  Miliki Mhandisi Masuhuko Nkuba pamoja na Mkuu wa Masoko na Uhusiano Bi. Lilian Mpanju Rugaitika katika ziara ya siku mbili iliyoanza  tarehe 19/05/2022.

Ziara hii ni mwendelezo wa ziara za Prof. Pallangyo zenye lengo la kufahamu Taasisi na utekelezaji wa majukumu mbalimbali, kwa kutembelea kampasi za TIA kufuatia uteuzi wake katika nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu mwezi, Machi 2022, ambapo akiwa Singida Afisa Mtendaji Mkuu alipokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kampasi kutoka kwa Meneja wa kampasi hiyo Dkt.James Mrema na taarifa ya miundombinu kutoka kwa Mhandisi Nkuba.

Wakati akimtambulisha Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Momole Kasambala aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo aliwashukuru wafanyakazi kwa ushirikiano na kuwataka kuendeleza ushirikiano huo kwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya.

Akiongea na Wafanyakazi, Afisa Mtendaji Mkuu alimshukuru Dkt. Kasambala kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi chote alichokaimu nafasi hiyo, huku akiwapongeza na kuwashukuru wafanyakazi walioitumikia TIA kwa muda mrefu akiwemo Mhadhiri Shisalalyandumi Ulomi.

Prof. Pallangyo ameendelea kuwasisitiza wafanyakazi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia dira, dhima, majukumu makuu ya Taasisi pamoja na Misingi ya Maadili ili kufikia malengo ya Taasisi kwa ufanisi zaidi.

Pia Prof. Pallangyo amefanya kikao na Serikali ya Wanafunzi (TIASO) Singida ambapo amepokea taarifa yao fupi na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi hao.

Awali, Prof. Pallangyo na ujumbe wake wakiongozwa na Meneja wa Kampasi ya Singida Dkt. James Mrema walifika kwenye Tamasha la Wanachuo la kuibua vipaji lililofanyika  tarehe 19/05/2022 katika ukumbi wa NLT Kampasi ya Singida.

 

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/