Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeendelea kupokea wadau mbalimbali kwenye Maonesho ya MAKISATU ambapo leo tarehe 19/5/2022, TIA imetembelewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Carolyne Nombo ambaye kabla ya uteuzi wake wa sasa alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu TIA, Profesa Nombo alikaribishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Wakili Said Musendo Chiguma pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa sasa Prof. William A. Pallangyo katika banda hilo.
Prof. Nombo ameipongeza TIA kwa kuendeleza jitihada za kujitangaza na kazi nzuri inayofanywa na Taasisi hasa upande wa utoaji huduma za Ushauri wa kitaalam. Pia ametoa wito kwa TIA kuhakikisha tunaendelea kutoa kozi zinazoendana na ujuzi unaohitajika kwenye soko la ajira
Katika Maonesho haya TIA inatoa huduma za Kozi zitolewazo kwa Wanafunzi waliochanguliwa na OR- Tamisemi kujiunga na TIA, pia kutoa maelekezo ya kina ya sifa za kujiunga kwa waliohitimu kidato cha Nne na cha Sita kwa miaka ya nyuma.