MICHEZO HUJENGA AFYA AKILIĀ 

December 14, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu Profesa William Pallangyo amewaasa wanachuo kuwa michezo ni furaha na Afya pia kwani kupitia michezo Afya ya akili uimarika sana hivyo kuwa chachu kubwa ya kufanya vizuri katika masomo yao,

“Pia wanamichezo muwe wabunifu kwa kutumiaĀ Ā mbinu mbalimbali za michezo ili kupata ushindi katika timu unayoichezea,”. Amsema Profesa Pallangyo

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania William Palangyo alipokutana na wanachuoĀ Ā waliowasili Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano ya SHIMIVUTA.

Wanachuo wa TIA watashindania tuzo mbalimbali kupitia michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, mpira wa wavu na riadha.

Naye Mlezi wa Wanachuo Lucina Comino amewasisitiza wanachuo hao kuepuka vitendo vyovyote ambavyo ni hatarishi katika kipindi chote watakachokuwa katika michezo hiyo,

“Tukiwa katika michezo yetu hii, nidhamu iwe ya hali ya juu na tutimize kile ambacho kimekusudiwa katika michezo na si tabia hatarishi ambazo zitaharibu sifa ya TIA,”. Alisema Madam Comino

Katika Michuoano inayoendelea Mechi za leo mpira wa miguu kati ya LGT naĀ Ā TIAĀ Ā huku TIA wakiibuka kidedea kwa goli 1, upande wa mpira wa kikapu TIA wameshinda kwa vikapu 53 dhidi ya Mw.nyerere vikapu 46.

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/