TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

MENEJA TIA KAMPASI YA MBEYA AWAASA WANAFUNZI KUFUATA SHERIA NA TARATIBU

October 26, 2022
Taasisi ya Uhasibu Tanzania ( TIA) Kampasi ya Mbeya, wameendelea kutoa maelekezo na taratibu mbalimbali za Utoaji wa Elimu, ushughulikiaji wa malalamiko, mazingira ya Chuo, utambulisho kwa wakuu wa idara wa Masomo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliowasili kwaajili ya kufanya Usajili.
Aidha TIA imetumia wiki hii kwa kutoa mafunzo namna ya kuepukana na rushwa na kujiepusha na udanganyifu wowote hasa katika kipindi cha mitihani.
Pia Dkt.Akyoo Meneja Kampasi ya Mbeya amewaasa Wanachuo hao kuzingatia taratibu na sheria kwa kuwa Taifa linahitaji vijana wazalendo na wenye maadili mwisho aliwakaribisha “Green City” na kuahidi kutoa ushirikiano mara tu watakapohitaji Ushauri kutoka kwake au kwa Wafanyakazi wa TIA.
 
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/