Leo tarehe 06/10/2022 aliyekuwa Kaimu Meneja Kampasi ya Kigoma CPA (T) Martin D. Mnyili amekabidhi Ofisi rasmi kwa Dkt. Florence W. Sitima kufuatia Uteuzi wake katika nafasi ya Kampasi Meneja Kigoma.
Makanidhiano hayo yamesimamiwa na Mwakilishi wa Meneja Rasilimali Watu Bi. Stella Manumbu na kushuhudiwa na Kaimu Ā Afisa Rasilimali Watu, TIA Kigoma Ā ndugu France D. Mwambene pamoja na Mkuu wa Taaluma ndugu Charles Merengo.
CPA (T) Mnyili amempongeza Dkt. Sitima kwa uteuzi huo na kumtakia mafanikio mema katika majukumu hayo mapya.
Naye Dkt. Sitima amemshukuru CPA (T) Mnyili kwa kazi nzuri aliyoifanya katika Kampasi ya Kigoma kwa kipindi chote alichokuwa akikaimu nafasi hiyo.
Baada ya Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Kampasi ya Kigoma zilizopo katika jengo la Red Cross , Dkt. Sitima alipata fursa ya kutembelea Eneo la Kampasi lililopo Kamala ambapo Taasisi inatarajia kuanza Ujenzi hivi karibuni.
“Kazi Iendelee”



