TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

KUAPISHWA KWA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI 

May 24, 2023
Tume ya Uchaguzi ya TIASO (Tanzania Institute of Accountancy Student Organization) jana tarehe 22/5/2023 ilimuapisha Rais wa serikali ya wanafunzi Bw.Sosteno A.Kweka na Makamu wa Rais Bi.Mwanaidi Issa na kupata wasaa wa kukutana na Menejimenti ya TIA.
Afisa Mtendaji Mkuu  Profesa.William Pallangyo alimpongeza Rais wa Serikali ya wanafunzi mteule,
 “Serikali ya Wanafunzi ni daraja kati ya Menejimenti na Wanachuo, ni muhimu Rais na Baraza la Mawaziri utakalolichagua kufuata  Katiba ya TIASO ili kuwaongoza wanachuo wenzenu kwa kanuni,  taratibu na sheria,”. Alisema Profesa Pallangyo
Pia Profesa Pallangyo amewaasa  Rais na Makamu wa  Rais wa TIASO kuwa mfano wa kuigwa na Wanachuo wenzao kwa maendeleo mazuri ya masuala ya taaluma, kuwa msaada wa haraka kwa Wanachuo wenzao kwa utatuzi wa changamoto au kutoa ushauri wenye tija.
Naye Makamu Mkuu wa chuo Taaluma,Tafiti na Ushauri Dkt.Momole Kasambala aliwaasa Viongozi hao kuwa mstari wa mbele kuimiza wanachuo wenzao kuhusu elimu ujuzi
“Mnapoenda kuanza majukumu yenu pamoja na Baraza la Mawaziri ni muhimu kusaidia wenzenu katika kuibua ujuzi,ubunifu mbaliambali, na kuhakikisha mnajiunga NACVET, pia baraza lenu la mawaziri lisiwe la kisiasa bali la kitaaluma na mkahimize wanafunzi kuepuka udanganyifu wakati wa mitihani na kulipa ada kwa wakati ili chuo kiweze kujiendesha,”. Alisema Dkt. Kasambala
 Aidha Dkt Issaya Hassanal aliwasihi viongozi wa serikali ya wanafunzi  kuacha makundi wasisahau wao ni viongozi wa wanafunzi wote na waepuke upendeleo,
“Kwanza nawapongeza sana kwa kuwa Viongozi wateule wa TIASO lakini sasa Kampeni umeisha na mmechaguliwa kwa demokrasia,  tunategemea ushirikiano mkubwa baina yenu na wanachuo wenzenu kwa maslahi mapana ya TIA,”. Alisema Dkt.Hassanal
Pia Mkurugenzi wa Huduma za wanafunzi Lucina Comino aliwapongeza Rais na Makamu wake na kuahidi kuwapa ushirikiano katika kipindi chote cha Uongozi wao.
Naye Rais wa Serikali ya wanafunzi Bw. Sosteno A. Kweka amesema anashukuru Mungu na wote waliokua nyuma yake hadi kuchaguliwa na ameahidi  kushirikiana vyema na uongozi wa TIA na kuwa mfano
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/