KATIBU TAWALA MKOA WA MWANZA AIPONGEZA TIA UJENZI WA KAMPASI YA MWANZA

June 11, 2022

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Ngusa Samike ameipongeza TIA kwa uwekezaji mkubwa wa kujenga Madarasa 9 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 1100, Jengo la utawala yenye ofisi 16, Maabara ya kisasa ya Kompyuta yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 200 pamoja na Maktaba kubwa ya kutumiwa na wanafunzi 250 kwa wakati katika Eneo la Nyang’homango Misungwi jijini Mwanza.

Mradi huo  unathamani ya shilingi za kitanzania bililoni 7.8 fedha  ambazo  TIA imefadhiliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi  Profesa William Pallangyo amesema TIA imejipanga kuendelea kuboresha miundombinu ya kusomea na kufundishia katika Kampasi zake zote ili kutoa elimu yenye ufanisi inayowaandaa wahitimu kujiajiri na kuajiriwa.

Katika Ziara hiyo Afisa Mtendaji Profesa Pallangyo pia ameambatana na Makamu Mkuu wa chuo anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri Dkt. Momole Kasambala, Mhandisi Miliki ndugu Masuhuko Nkuba na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Bi Lilian Rugaitika  wakiongozwa na Mwenyeji wao Dkt. Honest Kimario ambaye ni Kampasi Meneja wa Mwanza.

Vision and Mission
Core Values
Main Functions
Why Choose TIA
MAB Members
Online Application
Online Registration
LMS

Dar campus

Mbeya Campus

Singida Campus

Mtwara Campus

Kigoma Campus

Mwanza Campus

Tanga campus

Zanzibar Campus

 

History

Services

TIA Journal

TIA Repository

Open Access DB

Subscribed DB

Catalog

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/