TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

KARIBU NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI BANDA LA TIA MAONESHO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR 

June 19, 2022

Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Abdul- Gulam Hussein ametembelea Banda la Taasisi ya Uhasibu (TIA) katika Maonesho  ya tatu ya Wiki ya Elimu ya Juu Zanzibar amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Prof. William A. Pallangyo pamoja na Menejimenti ya TIA kwa kuamua kuanzisha Kampasi Makunduchi Shehia ya Kajengwa Mtaa wa Shungi Zanzibar amesema hii itawawezesha Wanafunzi wengi ambao walikuwa na lengo la kujiunga na TIA kuweza kutimiza ndoto zao za Elimu na kuwapunguzia Wazazi na Walezi gharama ambazo hulazimika kusomesha vijana wao Tanzania Bara.

 

 

/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/