TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY

KARIBU MAKAMU MKUU WA CHUO BANDA LA TIA

June 10, 2022
Makamu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Epaphra Manamba  atembelea Banda la Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu katika maonesho ya Mafunzo ya Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) yanayoendelea katika Viwanja vya Jamhuri, Dodoma.
Akiwa katika Banda hilo Wafanyakazi wa TIA wakiongozwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Bi. Lilian Rugatika kwa pamoja walimpongeza Profesa Manamba kwa uandishi wa kitabu cha “Quantitative Methods for Economics and Finance”.
Karibu katika Banda hili utapata huduma za Udahili kama Kozi zinazotolewa,ushauri wa kozi za kusoma kulingana na ufaulu wa Mwanafunzi kuanzia ngazi ya cheti cha awali, Stashahada, Shahada ya Kwanza, Stashahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamili, pia utapata huduma za Utafiti na Ushauri wa kitaalam.
/*** Collapse the mobile menu - WPress Doctor ****/