Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara wa  Taasisi ya Uhasibu Tanzania Wakili Said Musendo Chiguma ameipongeza TIA kwa mara ya kwanza kushiriki Maonesho ya Nane Nane kanda ya Kaskazini Arusha yanayowezesha kukutana na wadau mbalimbali
“Hakika hongereni sana kwa kuendelea kuitangaza TIA, nimefarijika kuwaona kanda hii ya Kaskazini mkishiriki maonesho haya yenye tija kubwa kwa Taasisi na kwa Wananchi tunaowahudumia kwani yanatukutanisha na wadau mbali mbali muhimu,”. Alisema Wakili Chiguma
Mwenyekiti wa Bodi amesema hayo alipotembelea banda la TIA katika maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika viwanja vya Themi Njiro, Arusha.

